

Lugha Nyingine
Reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung yatimiza siku 100 tangu kuanza kazi huku abiria milioni 1.45 wakisafirishwa (3)
![]() |
Abiria wakionekana katika picha kwenye ukumbi wa kusubiria treni wa Stesheni ya Halim ya Reli ya Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung (HSR) mjini Jakarta, Indonesia, Januari 24, 2024. (Xinhua/Xu Qin) |
JAKARTA - Reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung (HSR) imeadhimisha kutimia siku yake ya 100 tangu kuanza kufanya kazi siku ya Jumatano ikiwa imesafirisha abiria jumla ya milioni 1.45, afisa kutoka Shirika la Kimataifa la Reli la China amesema huku akiongeza kuwa ratiba za treni zimerekebishwa na kuboreshwa ili kuendana na sikukuu za jadi za nchi hiyo na hali ya mtiririko wa abiria ili kuboresha uwezo wa usafirishaji.
Idadi ya safari za treni za kila siku imeongezwa kutoka 14 hadi 40, na 48 wikendi. Safari jumla ya 3,487 zimeendeshwa ndani ya siku hizo 100 za kwanza tangu kuanza kufanya kazi, na idadi kubwa zaidi ya abiria waliosafiri kwa siku moja ilikuwa 21,537, huku kiwango cha juu zaidi cha tiketi zilizonunuliwa kwa siku kilichorekodiwa kilikuwa asilimia 99.6, afisa huyo amesema.
Wakati huo huo, reli hiyo iliyojengwa na China imeboresha vifaa na huduma zake kwenye stesheni zake ili kuwapa abiria uzoefu mzuri na wa kufurahisha wa kusafiri. Migahawa zaidi ya vyakula vya haraka, maduka ya vinywaji, na maduka ya kununua kwa urahisi yanapatikana katika stesheni za Halim, Padalarang na Tegalluar. Treni hiyo ina vifaa visivyo na vizuizi ili kukidhi mahitaji ya abiria tofauti.
Septian Hario Seto, Naibu Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Baharini na Uwekezaji ya Indonesia, amesema reli hiyo imeleta mageuzi makubwa katika usafiri kati ya Jakarta na Bandung, ikihamisha wasafiri kutoka kutegemea usafiri wa barabara kuu hadi reli.
"Nina hakika kwamba katika siku zijazo, mtindo wetu wa usafirishaji utabadilika kutoka kwa usafiri wa mtu binafsi hadi usafiri wa umma. Ndiyo maana tuna shauku ya kupanua ushirikiano wetu na kupanua reli ya mwendo kasi kutoka Jakarta hadi Surabaya kupitia Yogyakarta," amesema.
Tangu reli hiyo ianze kufanya kazi kibiashara Oktoba 2023, muda wa kusafiri kati ya Jakarta na Bandung umepunguzwa kutoka saa zaidi ya tatu hadi dakika 46, ikitoa machaguo zaidi kwa watalii, watu wanaosafiri kila siku na familia zenye watu wanaoishi maeneo tofauti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma