Viongozi wa Afrika watoa wito wa kuharakisha maendeleo ya viwanda ili kufikia ustawi (2)

(CRI Online) Januari 29, 2024
Viongozi wa Afrika watoa wito wa kuharakisha maendeleo ya viwanda ili kufikia ustawi
Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo akiongea kwenye Mazungumzo kuhusu Ustawi wa Afrika tarehe 27, Januari. (Picha na Seth/Xinhua)

Mazungumzo kuhusu Ustawi wa Afrika yanayotarajiwa kufikia tamati leo Jumatatu ambayo yalifungwa Januari 27 nchini Ghana, yameshushuhudia viongozi wa Afrika walioshiriki wakitoa wito kwa nchi za Afrika kushikamana na kushirikiana katika kupiga jeki maendeleo ya viwanda barani Afrika ili kufikia ustawi.

Kwenye mazungumzo hayo, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amesema nchi za Afrika zinahitaji kujenga miundombinu yenye ufanisi ya uchukuzi na ugavi, kurahisisha biashara, kueneza matumizi ya teknolojia za kidijitali kwenye miamala ya kimataifa, na kuchochea biashara kati ya nchi za Afrika.

Amesema, utekelezaji wa sasa wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) umetoa fursa nyingi zaidi kwa biashara za kuvuka mpaka, na unatarajiwa kuchangia ukuaji wa uchumi na kulijenga Bara la Afrika lenye mafungamano zaidi.

Mazungumzo hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo Sekretarieti ya AfCFTA, yanalenga kuweka jukwaa la mawasiliano kwa wanasiasa na wafanyabiashara wa Afrika, kwa lengo la kutafuta njia ya kufikia ustawi wa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha