Dubu pori weusi katika Mji wa “Ncha ya Mashariki ya China” wavutia watalii (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2024
Dubu pori weusi katika Mji wa “Ncha ya Mashariki ya China” wavutia watalii
Picha ikionehsa dubu pori weusi wakiangaliana na watalii walio ndani ya gari kwenye Bustani ya Dubu Pori katika Kisiwa cha Heixiazi kilichoko Mji wa Fuyuan, Mkoa wa Heilongjiang, China, tarehe 25, Januari. (Picha na Wang Yuguo/Xinhua)

Katika hali ya hewa ya baridi kali ya karibu nyuzi joto 30 chini ya sifuri mjini Fuyuan, ambao unasifiwa kama “Ncha ya Mashariki mwa China", Mto karibu na Kisiwa cha Heixiazi umefunikwa na theluji nene.

Kisiwa cha Heixiazi (jina la utani la dubu weusi katika lugha ya Kichina) kilipewa jina lake kutokana na dubu pori weusi wengi ambao walikuwa wakizunguka kwenye kisiwa hicho. Kipo kwenye makukutano ya Mto Heilongjiang na Mto Ussuri, kwenye mpaka kati ya China na Russia.

Kwa mujibu wa takwimu ya idadi ya watalii waliopokelewa katika eneo la kitalii la Kisiwa cha Heixiazi, kutoka mwanzoni mwa mwaka jana hadi kipindi cha Sikukuu ya mbalamwezi na Siku ya Taifa la China mwaka jana (mwanzoni mwa mwezi Oktoba), eneo hilo la kitalii lilipokea watalii laki 1.5, idadi ambayo ilikuwa ni maradufu kuliko mwaka uliotangulia, ikiashiria ongezeko jipya katika ustawi wa utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha