

Lugha Nyingine
Maandamano ya wakulima wa Ufaransa yafunga barabara kuu kuzunguka Paris
![]() |
Wakulima wa Ufaransa wakiwa wamefunga barabara kuu kwa kutumia matrekta yao kwenye maandamano huko Longvilliers, karibu na Paris, Ufaransa, Januari 29, 2024. (Picha na Aurelien Morissard/Xinhua) |
PARIS - Wakulima wa Ufaransa wamefunga barabara zinazozunguka Mji wa Paris siku ya Jumatatu alasiri wakati wakiendelea kupinga kupanda kwa bei, urasimu na "ushindani usio wa haki" kutoka nchi nyingine ambapo "vizuizi" vinane vimewekwa kwenye barabara kuu za kuzunguka mji mkuu huo wa Ufaransa.
Matrekta takriban 800 yamezunguka mji huo, huku wakulima wakiapa "kuipa njaa Paris." Kwa mujibu wa jeshi la polisi, idara 30 na barabara kuu 16 zimeathiriwa na harakati za wakulima hao kote nchini Ufaransa.
Wakulima wa Ufaransa walianza harakati zao karibu wiki mbili zilizopita ili kuandamana dhidi ya kupungua kwa mapato na kuongezeka kwa sheria, kanuni na kazi za mafailii. Baadhi wanalalamika kuwa sera za biashara zisizo za haki zimewaweka katika ushindani usio sawa na wakulima kutoka nchi nyingine wasiofuata na sheria sawa.
Waziri wa Kilimo wa Ufaransa Marc Fesneau ametangaza kuwa "hatua mpya zitachukuliwa kesho (Leo Jumanne)." Wakati huo huo, Rais Emmanuel Macron aliitisha mkutano na mawaziri kadhaa Jumatatu alasiri kujadili hali hiyo, ofisi yake ilisema.
Waziri Mkuu Gabriel Attal alikuwa ametangaza hatua kadhaa za awali kuitikia hasira za wakulima, ikiwa ni pamoja na kusimamisha kupanda kwa gharama ya dizeli kwa matumizi ya mashine za shambani. Pia ameahidi kurahisisha kazi za kiutawala kwa wakulima na kutoa ruzuku katika kilimo cha kioganiki. Hata hivyo, hatua hizi hazikuzima hasira za wakulima.
Attal alisema Jumapili kwamba hatua hizo za awali zilikuwa ni "mwanzo tu," na kuahidi "kuendelea siku baada ya siku, wiki baada ya wiki, kupiga hatua ya maendeleo."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma