

Lugha Nyingine
Mabadilishano ya kitamaduni yaangaziwa katika sherehe za mwaka mpya wa jadi wa China nchini Uganda (6)
![]() |
Watu wakitazama burudani ya zana za muziki za kijadi za China kwenye Gulio la Mwaka Mpya wa Jadi wa China mjini Kampala, Uganda, Januari 28, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua) |
KAMPALA –Wachina na Waganda walishiriki katika onyesho la mchezo wa Tai Chi siku ya Jumapili kwenye sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ilikuwa ishara ya kuimarika kwa uhusiano kati ya watu wa nchi hizo mbili wakati ambapo maelfu ya Waganda na jamii ya Wachina walikusanyika katika uwanja wa Uhuru wa Kololo mjini Kampala kwa ajili ya "Gulio la Mwaka Mpya wa Jadi wa China," shughuli ya kitamaduni inayohusisha kila aina ya sanaa za kijadi za China na kufuatiwa na tamasha la burudani jioni, ili kusherehehea Mwaka mpya ujao wa jadi wa China wa Dragoni, au Sikukuu ya Sping ambayo itaangukia Februari 10 mwaka huu.
Ngoma za simba na maonyesho ya kibunifu yaliyochanganya mambo ya kitamaduni ya Uganda na China yaliwaduwaza watazamaji. Harufu nzuri za vyakula vya Kichina na milo ya nchi nyingine zilijaa mahali hapo.
Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong amesema Sikukuu ya Spring ni sikukuu muhimu zaidi ya jadi ya Wachina, inayojumuisha mkusanyiko wa familia na kutakia heri kwa mwaka ujao. "Siyo tu inabeba dhana za ustaarabu wa China wa amani na masilikizano lakini pia inabeba maadili ya kawaida ya binadamu kama vile familia yenye usawa, ujumuishaji wa kijamii, na uhusiano mzuri kati ya binadamu na mazingira ya asili."
Ametoa wito kwa Wachina wanaoishi nchini Uganda "kutekeleza kikamilifu majukumu ya kijamii ya kampuni na kuhimiza urafiki baina ya watu wa China na Afrika."
Henry Okello Oryem, Waziri wa Nchi kwa Mambo ya Kimataifa wa Uganda, amesema Afrika ina uhusiano maalum wa kihistoria na China, ambao ulikuwa na mchango mkubwa katika kusaidia nchi za kusini mwa Afrika, hasa, kupambana na ukoloni.
Amesema China imefadhili ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu ya uchukuzi na nishati, ambayo imehimiza maendeleo ya viwanda ya nchi yake pamoja na ukuaji wa kijamii na kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma