Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia (8)

By Zhao Jian (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2024
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia

Kisiwa cha Kulangsu kilichoko Mji wa Xiamen, Mkoa wa Fujian, China siyo tu ni “bustani ya baharini” yenye hali nzuri ya hewa kama majira ya mchipuko kwa mwaka mzima, bali pia kimesifiwa kama “Makumbusho ya Usanifu Majengo ya Mataifa mbalimbali” kwa sababu ya majengo yake mengi makongwe kiliyo nayo, ambayo yanavutia watalii kutoka ndani na nje ya China.

Historia ya Kisiwa cha Kulangsu imeleta mandhari ya kipekee ya kiutamaduni. Kuanzia mwaka 1844, nchi 13 zilianzisha ubalozi mdogo katika kisiwa hicho, na Uingereza, Marekani, Ufaransa na nchi nyingine pia zilijenga makanisa, kufungua shule, hospitali, maduka n.k. huko Kulangsu.

Kwa sasa kuna majengo makongwe zaidi ya 1,000 yenye usanifu wa aina mbalimbali yaliyojengwa kisiwani hapo kuanzia mwishoni mwa karne ya 19 hadi nusu ya kwanza ya karne ya 20. Mengi ya majengo hayo, yanachanganya usanifu wa Magharibi pamoja na umaalum wa usanifu wa kijadi wa China.

Kamati ya Urithi wa Dunia inaamini kuwa, Kisiwa cha Kulangsu kimeshuhudia historia ya kuelewana na maendeleo ya pamoja kati ya tamaduni mbalimbali na maadili tofauti Duniani, na kinatoa rejea kwa maendeleo jumuishi ya tamaduni tofauti za China na sehemu nyingine.

Tarehe 8, Julai 2017, mradi wa “Kulangsu: Jumuiya ya Kihistoria ya Kimataifa” uliorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia, ukiwa mradi wa 52 wa China kwenye orodha hiyo.

(Picha na Wu Chaolan, Su Yingxiang/People's Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha