

Lugha Nyingine
Nyasi za Juncao zilizogunduliwa na Wanasayansi wa China zaleta faida kwa wafugaji wa ng'ombe wa maziwa nchini Kenya (6)
![]() |
Wakulima wakiponda mazao ya nyasi za Juncao kwenye shamba la Juncao katika Kijiji cha Lenginet, Nakuru, Kenya, Januari 26, 2024. (Xinhua/Han Xu) |
NAIROBI - Nyasi za kijani kibichi, ndefu na nene katika shamba kubwa la Juncao katika Kaunti ya Nakuru Kaskazini-Magharibi mwa Kenya zilikuwa zikivuma kwa mawimbi ya upepo Ijumaa alasiri, na kuleta mandhari nzuri. Zikiwa zilipandwa na mfanyabiashara wa China Jack Liu Mwaka 2021, nyasi hizo zimeleta mabadiliko makubwa katika ufugaji wa mifugo wa maeneo ya nusu ukame nchini Kenya, na hivyo kutoa hakikisho la usambazaji usiokoma wa malisho ya mifugo kwa wafugaji na wakulima wadogo wadogo.
Ndani ya shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 50 (kama hekta 20), kikundi cha wakulima na wafanyakazi wenyeji walikuwa wakitembea-tembea huku wakifurahia mazingira na kuona nyasi ndefu za zaidi ya mita sita ambazo zimeshinda mazingira magumu na kuchanua.
Katika wiki kadhaa zilizopita, Francis Fwamba Wanambisi, mfugaji wa ng'ombe wa maziwa mwenye umri wa miaka 60, amekuwa akitembelea shamba hilo mara kwa mara ambapo amekuwa akinunua nyasi za Juncao kwa gharama nafuu ili kulisha ng'ombe wake tisa.
"Hadi sasa nimenunua nyasi hizi mara tatu tangu mwanzo wa mwaka na nimeshuhudia kuboreka kwa kiasi kikubwa kwa ng'ombe wangu. Uzalishaji wao wa maziwa umeongezeka maradufu," Wanambisi ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika shamba hilo.
Ng’ombe wake watatuwalilishwa nyumbani na alipoanza kuwalisha nyasi hizo, kila mmoja alianza kutoa lita tano na nusu za maziwa asubuhi, kutoka karibu lita tatu za awali.
Wanambisi alifahamu kuhusu nyasi za Juncao kutoka kwa wenzao ambao walisifu juu ya virutubisho vyake vya lishe bora ikiwa ni pamoja na protini ambazo ni muhimu kwa uzalishaji mkubwa wa maziwa miongoni mwa mifugo ya ng'ombe wa kienyeji.
Huku ng'ombe wake sasa wakizalisha maziwa mengi, baba huyo wa watoto wanane amesema anauza ziada katika kituo cha maduka cha eneo hilo, na kupata mapato makubwa ya kukimu familia yake.
Liu, afisa mtendaji mkuu na mwanzilishi wa shamba hilo, amesema limekuwa mfano wa kuigwa kwa uzalishaji endelevu wa chakula cha ng'ombe nchini Kenya, kupitia kutumia teknolojia ya China ya gharama nafuu lakini inayoweza kuendana na mazingira ya Kenya.
"Sisi tumejikita mahsusi katika mashamba ya nyasi za Juncao, tukisambaza malisho ya mifugo kwa wafugaji wenyeji," Liu amesema.
Zikiwa zinalimwa katika nchi zaidi ya 100 duniani kote na kupata mvuto barani Afrika, nyasi za Juncao ziligunduliwa na kuanzishwa na wanasayansi wa China katika Mkoa wa Fujian katika miaka ya 1980, na zina sifa bora zaidi ikiwa ni pamoja na urefu, majani mapana na mashina yenye sukari nyingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma