Kutoka ziwa lenye harufu kali hadi “Mapafu ya kijani ya Mji”: Mabadiliko ya kushangaza ya Ziwa Yundang

By Wu Chaolan, Zhao Jian (Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2024
Kutoka ziwa lenye harufu kali hadi “Mapafu ya kijani ya Mji”: Mabadiliko ya kushangaza ya Ziwa Yundang
Picha ya juu: Ziwa Yundang kabla ya kusafishwa. Picha ya chini: Ziwa Yundang lilivyo hivi sasa.

Mwishoni mwa miaka ya 1980, Ziwa Yundang lililoko Mji wa Xiamen, Mkoa wa Fujian wa China lilikuwa limejaa magugu, takataka zilitapakaa kila mahali, mbu na nzi walikuwa wakizaliana kwa wingi, na ndege, samaki na kamba walikuwa karibia kutoweka. Lilikuwa ziwa lenye harufu kali na mazingira mabaya.

Mwaka 1988, serikali ya Mji wa Xiamen ilitoa sera ya “Kusimamia ziwa kwa mujibu wa sheria, kushughulikia na kuondoa majitaka na matope, kusafisha maji na kujenga kingo, na kuboresha mazingira ya asili”, sera hiyo ambayo ilitoa mwelekeo kwa utekelezaji wa hatua mbalimbali za usimamizi wa Ziwa Yundang tangu hapo.

Hivi leo ukubwa wa eneo linalozunguka Ziwa Yundang umefikia kilomita za mraba 2.6, na bioanuai yake inaendelea kuongezeka. Makundi ya ndege yangeyange na ndege wengine wanakuja na kuishi hapa. Njia za watembea kwa miguu kuzunguka ziwa hilo, uoto wa mikoko na sehemu ya kuhifadhi ndege yangeyange, vyote vimekuwa mandhari ya kuvutia ya Mji wa Xiamen, na eneo la Ziwa Yundang limepata sifa ya kuwa “Sebule ya Mji”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha