Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2024
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika karibu na lango la Ziwa Yundang huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (Picha imetolewa kwa People’s Daily Online)

Miongo kadhaa iliyopita, Ziwa Yundang, lililo katikati ya Xiamen, Mkoa wa Fujian, China lilikuwa limeathiriwa na uchafuzi wa mazingira. Baada ya kufanya juhudi kwa miaka mingi katika kuhifadhi mazingira tangu miaka ya 1980, ziwa hilo limepitia mabadiliko ya ajabu na kuwa mazingira ya utulivu na yenye mandhari ya kuvutia mjini humo yaliyo kama kimbilio la mazingira ya asili katikati ya majengo marefu.

Ndani ya rasi, visiwa vidogo vyenye uoto wa kijani vimekuwa makazi ya ndege yangeyange, ndege ambao ni alama ya Xiamen. Mandhari hiyo ya kuvutia siyo tu inatoa mapumziko tulivu kwa wakazi wa eneo hilo lakini pia yamekuwa sehemu ya kuvutia kwa watazamaji wa ndege na wapiga picha wanaomiminika ili kupiga picha nzuri za ndege hawa katika mazingira yao ya asili.

Peng Zhiwei, Mkuu Shirikisho la Waangalizi wa Ndege la Xiamen, ametoa mkusanyiko wa picha alizopiga za yangeyange hao waliopendeza kwa People's Daily Online. Mkusanyiko wake huo wa picha hutumika kama ushuhuda kamili wa uhifadhi wa mazingira uliofanikiwa wa Ziwa Yundang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha