Mauzo kwenye Soko la samaki lenye historia ya miaka mia yashamiri wakati Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2024
Mauzo kwenye Soko la samaki lenye historia ya miaka mia yashamiri wakati Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia
Mfanyabiashara akifungasha samaki walioganda kwenye soko la samaki la “ncha ya mashariki mwa China” tarehe 31, Januari.

Wakati mwaka mpya wa jadi wa China unapokaribia, soko la samaki la “Ncha ya Mashariki mwa China” katika Mji wa Fuyuan, Mkoa wa Heilongjiang, linalojulikana kama “Mji Mkuu wa Samaki Wabichi wa China” limeingia msimu wake wa mauzo mengi. Soko la Samaki la Mji wa Fuyuan lilianzishwa katika zama za kale na limekuwa na historia ya zaidi ya miaka mia. Kwa sasa soko hilo limekuwa moja kati ya sehemu muhimu zaidi za usambazaji wa bidhaa za samaki wabichi nchini kote China.

Picha na Wang Jianwei/Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha