Waandamanaji wafunga barabara karibu na mkutano wa kilele wa EU mjini Brussels

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2024
Waandamanaji wafunga barabara karibu na mkutano wa kilele wa EU mjini Brussels
Matrekta yakiwa yamefunga barabara wakati wa maandamano huko Brussels, Ubelgiji, Februari 1, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

BRUSSELS – Polisi wamesema, kwa kuitikia wito wa muungano wa wakulima wa Ulaya, Uratibu wa Ulaya kupitia Campesina (ECVC), wakulima waandamanaji wamefunga barabara kwa kutumia matrekta takribani 1,300 kuzunguka eneo la mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya (EU) ambapo viongozi 27 wa umoja huo wamekusanyika siku ya Alhamisi, ambapo wakulima walikusanyika saa 5 asubuhi kwa saa za huko (1000 GMT) kwenye jengo la Place du Luxembourg mjini Brussels, eneo ambalo Bunge la Ulaya lililoko.

Eneo hilo liko umbali wa kilomita moja kutoka kwa mzunguko wa barabara wa Schuman, ambapo mkutano maalum wa kilele wa EU unafanyika.

Waandamanaji hao wameeleza malalamiko yao kuhusu kodi, mzigo mkubwa wa kiutawala, kupanda kwa gharama na bei nafuu ya bidhaa za kilimo zinazoingizwa Ulaya, na wakaomba viongozi wa EU kutoa msaada zaidi.

"Sera za uliberali mamboleo za Ulaya zinahusika kwa kiasi kikubwa na matatizo ya wakulima: mikataba ya biashara huria (FTAs), kupunguza udhibiti wa soko, ruzuku ya Sera ya Pamoja ya Kilimo (CAP) ambayo inasambazwa kwa njia isiyo ya haki kabisa, mzigo wa kiutawala, suluhu lisilo la halisi kama vile msaada usio na maana kwa mambo ya kidijitali, GMOs na masoko ya kaboni, na ukosefu wa dira ya jumla ya kuhamia kwenye njia endelevu zaidi za kilimo,," ECVC imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

ECVC inadai kufuta FTA zinazohusishwa na kilimo pamoja na kusitisha mazungumzo kati ya EU na jumuiya ya biashara ya Amerika Kusini Mercosur, kutoa bei za haki za mazao ya shambani huku kukiwa na kupanda kwa gharama za uzalishaji, ugawaji upya wa ruzuku za Sera ya Pamoja ya Kilimo (CAP) kwa kila mfanyakazi anayefanya kazi badala ya kwa hekta ili kusaidia vyema mashamba madogo na ya kati wakati wa kuhamia kuelekea kilimo cha kiikolojia na uendelevu, na kurahisisha urasimu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha