Lugha Nyingine
Njia ya kutazama mandhari ya treni ya Maglev yashamirisha utalii katika mji wa kale wa Fenghuang, China
FENGHUANG - Njia ya kutazama mandhari ya treni ya Maglev ya Fenghuang ilifunguliwa rasmi Julai 30, 2022. Njia hiyo inaanzia stesheni ya mji wa kale cha Fenghuang, ikiwa na urefu wa kilomita 9.121, ikiunganisha maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii katika mji wa kale wa Fenghuang katika mji unaojiendesha wa Makabila ya Watujia na Wamiao wa Xiangxi, Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China. Abiria wanaweza kufurahia mandhari nzuri nje ya madirisha ya treni wakiwa njiani.
Wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China, treni hiyo ya Maglev ya Fenghuang inatarajiwa kusafirisha abiria zaidi ya 10,000 kila siku.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma