Sherehe ya kipekee yafanyika kwa ajili ya Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa Tibet

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2024
Sherehe ya kipekee yafanyika kwa ajili ya Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa Tibet
Msanii akichangamana na watoto wakati wa sherehe katika duka la vitabu mjini Lhasa, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China, Februari 3, 2024. (Picha na Tenzin Nyida/Xinhua)

Sherehe ya kipekee imefanyika siku ya Jumamosi katika duka la vitabu vya watoto katika Mji wa Lhasa, ambapo walimu walitambulisha na kufahamisha mila na desturi za kijadi za Mwaka Mpya wa Jadi wa Tibet. Kwenye sherehe hiyo, watoto waliovalia mavazi ya kijadi ya Kitibet walifurahia maonyesho ya muziki, maonyesho ya vikaragosi na utengenezaji wa kazi za mikono, pamoja na karamu ya "gutu", chakula cha kijadi cha supu kinachotengenezwa kwa unga wa ngano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha