Mradi wa bandari ya uvuvi ambao ni msaada wa China kwa Ghana wakamilika kwa asilimia 88

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2024
Mradi wa bandari ya uvuvi ambao ni msaada wa China kwa Ghana wakamilika kwa asilimia 88
Picha hii iliyopigwa Februari 6, 2024 ikionyesha eneo la ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Jamestown ambayo ni msaada wa China kwa Ghana huko Accra, mji mkuu wa Ghana. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA - Mkandarasi wa China anayejenga mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Jamestown ambayo ni msaada wa China kwa Ghana amesema siku ya Jumanne kuwa karibu asilimia 88 ya ujenzi wa mradi huo umekamilika kwa ujenzi wa gati jipya, ambalo ni sehemu kuu ya bandari hiyo ya uvuvi.

Jin Xiaodong, meneja mkuu wa mradi huo, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano kwamba gati hilo jipya liko tayari kuendeshwa kikamilifu pindi bandari hiyo ya uvuvi itakapokamilika.

Katika eneo la ujenzi mashine zinaunguruma na majengo makuu likiwemo soko la wavuvi tayari yameanza kuwa na mwonekano wake wa usanifu.

"Shukrani kwa bidii ya wafanyakazi wa China na Ghana, ujenzi wa mradi umeingia katika kipindi chake cha mwisho," Jin amesema.

Jin amesema, mradi huo unaosaidiwa na China utakuza kwa kiasi kikubwa sekta ya uvuvi ya Ghana na maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo katika muda mrefu.

"Pia ni daraja la urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili," amesema.

Mradi huo unaosaidiwa na China ulianza kujengwa Mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha