Fataki zaidi ya 70,000 zarushwa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, na Xiamen na Kinmen "zamulika" kwa fashifashi anga la mkesha wa Mwaka Mpya kwa wakati mmoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2024
Fataki zaidi ya 70,000 zarushwa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, na Xiamen na Kinmen
Xiamen na Kinmen zikisherehekea kwa pamoja Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa fashifashi za fataki. (Picha na Chen Wenqi)

Tamasha la Fashifashi za Fataki ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ya Kuvuka Mlango Bahari wa Taiwan Mwaka 2024 lilifanyika kwa wakati mmoja Jioni ya Februari 10, katika Miji ya Xiamen na Kinmen. Usiku huo, fataki zaidi ya 70,000 zenye kutoa fashifashi za kung'aa zilipaa angani kutoka Ufukwe wa Huangcuo wa Mtaa wa Huandao katika Fukwe ya Xiaojinmen huko Xiamen, zikiangaza anga la Mkesha wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan.

Habari zilisema kwamba tangu Mwaka 1987, Xiamen na Kinmen zilianza kufyatua fataki za fashifashi kwa pamoja ili kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na utaratibu huu unaendelea hadi leo. Kwa sababu hii, katika usiku wa kwanza wa mwezi wa kwanza wa mwaka mpya kwa kalenda ya kilimo ya China, kufurahia fashifashi kutoka pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan na kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi kwa pamoja vimekuwa moja ya shughuli muhimu za Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China huko Xiamen na Kinmen.

Tamasha hilo la fashifashi limeandaliwa na Serikali ya Mji wa Xiamen na Serikali ya Wilaya ya Kinmen, na kusimamiwa na Serikali ya Eneo la Siming na Idara ya Usafirishaji na Utalii ya Wilaya ya Kinmen.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha