Hong Kong yafanya maonyesho ya fashifashi za fataki kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2024
Hong Kong yafanya maonyesho ya fashifashi za fataki kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Fashifashi za fataki katika kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ziking’arisha anga juu ya Bandari ya Victoria huko Hong Kong, Kusini mwa China, Februari 11, 2024. (Xinhua/Zhu Wei)

HONG KONG -Baada ya kutofanyika kwa miaka minne tangu Mwaka 2020, Maonyesho ya Fashifashi za Fataki ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China 2024 kwa mara nyingine tena yameng’arisha anga la usiku la Bandari ya Victoria ya Hong Kong siku ya Jumapili kuanzia saa 2 usiku kwa saa za huko (1200 GMT), ili kushrehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Maonyesho hayo yalipangiwa na Idara ya Utamaduni, Michezo na Utalii ya serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) na kufadhiliwa na Shirikisho la Sherehe la Hong Kong.

Kaulimbiu ya maonyesho hayo ya mwaka huu ni "Biashara zote zinastawi, na China inasimama kidete katika zama za ustawi." Fataki kutoka mifyatuo 23,888 ya pyrotechnic zilirushwa kutoka kwenye majahazi matatu katika dakika 23 za nderemo, kwa jumla kulikuwa na maonesho manane ya fashifashi za fataki.

Tam Kam-kau, Mwenyekiti wa Shirikisho la Sherehe la Hong Kong, amesema kuwa fashifashi za fataki za mwaka huu zimeonyesha miundo maalum ya kutuma salamu za Mwaka Mpya wa jadi kwa watu wa Hong Kong na watalii, na kuitakia Hong Kong kusonga mbele kwa hatua madhubuti katika safari mpya kutoka kwenye utulivu hadi ustawi.

Pande mbili za bandari ya Victoria zikiwa pamoja na Tsim Sha Tsui na Wan Chai zilikuwa zimejaa watu waliotazama maonesho ya fashifashi. Katika baadhi ya maeneo yenye mandhari nzuri, watu walikuwa wamesubiri kwa saa kadhaa kabla ya maonyesho hayo kuanza.

"Maonesho hayo ya fashifashi ni mazuri zaidi katika historia yake, na rangi zao ni murua sana !" Mkazi wa Hong Kong Bi Cheung alisema.

Akizungumza katika hafla iliyoandalliwa na Shirikisho la Sherehe la Hong Kong kabla ya maonyesho hayo, John Lee, afisa mtendaji mkuu wa HKSAR, amesema kuwa dragoni anawakilisha furaha na uhai. Ana imani kwamba Hong Kong itastawi katika Mwaka wa Dragoni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha