Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2024
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Ndege ya abiria ya C919 ambayo ni ya kwanza kuundwa na China kwa kujitegemea ikifanya safari ya mazoezi kujiandaa kwa Maonyesho yajayo ya Anga ya Singapore (Singapore Airshow), Februari 18, 2024. (Picha na Then Chih Wey/Xinhua)

SINGAPORE - Ndege ya abiria ya C919 ambayo ni ya kwanza kuundwa na China kwa kujitegemea imefanya safari ya mazoezi siku ya Jumapili nchini Singapore kujiandaa kwa ajili ya Maonyesho yajayo ya Anga ya Singapore (Singapore Airshows) ambapo ndege tano zilizoundwa na Shirika la Ndege ya kibiashara la China, ikiwa ni pamoja na C919, zitakutana na umma kwenye maonyesho hayo.

C919 itafanya maonyesho ya safari za ndege katika Maonyesho ya Anga ya Singapore Mwaka 2024 (Singapore Airshow 2024), ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 20 hadi 25 Februari.

Maonyesho hayo yanashirikishwa na timu za kufanya maonyesho ya kuchezesha ndege angani kutoka India, Australia, Indonesia na Korea Kusini.

Jeshi la Anga la Singapore litatuma ndege yake ya kivita ya F-15 na helikopta ya mashambulizi ya Apache kwenye maonyesho hayo.

Shughuli hiyo, itakayoshirikishwa na kampuni zaidi ya 1,000, inatarajiwa kuvutia washiriki wa kibiashara 50,000 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 50.

Maonyesho hayo yataweka banda la nchi kwa kampuni za vyombo vya safari za anga za China kwa mara ya kwanza, kwa mujibu wa waandaaji. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha