

Lugha Nyingine
Ziwa Yundang huko Xiamen, China lashuhudia mageuzi ya kiikolojia
Katika miaka ya 1970, watu walipanua eneo la ardhi kwa kuzuia bahari ili kuongeza uzalishaji wa nafaka, na Yundang ikawa ziwa. Kadri idadi ya watu na viwanda ilipoongezeka, uchafuzi wa maji uliongezeka kwa kasi. Maji taka kutoka kwa viwanda zaidi ya 100 yalimwagwa moja kwa moja ndani ya ziwa hilo, pamoja na maji taka ambayo hayajasafishwa kutoka kwa mamia ya maelfu ya wakazi wa eneo hilo.
Katikati ya miaka ya 1980, hatua mbalimbali zilitekelezwa ili kubadilisha mwenendo huo na kurejesha ziwa katika hali yake nzuri ya awali. Viwanda vya kampuni karibu na ziwa vyote vilifungwa na kuhamishwa, mitambo ya maji taka ilijengwa, na maji ya bahari yalielekezwa ndani ya ziwa ili kuleta uhai wa maji.
Kwa juhudi hizo katika miaka zaidi ya 30 iliyopita, Ziwa Yundang, sasa lina maji safi na viumbe vingi vya majini, likitumika kama eneo lenye mandhari nzuri kwa wakazi na watalii sawia. (Xinhua/Jiang Kehong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma