China yashinda taji la Dunia la mpira wa mezani kwa wanaume kwa mara ya 11 mfululizo kwenye mashindano ya Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2024
China yashinda taji la Dunia la mpira wa mezani kwa wanaume kwa mara ya 11 mfululizo kwenye mashindano ya Dunia
Timu ya China ikishangilia na kombe kwenye hafla ya kukabidhiwa kombe la ushindi kwa timu ya wanaume kwenye Fainali za Mashindano ya Mpira wa Mezani ya Timu ya Dunia ya Shirikisho la Mpira wa Mezani Duniani - ITTF Busan 2024 mjini Busan, Korea Kusini, Februari 25, 2024. (Xinhua/Yang Shiyao)

BUSAN, Korea Kusini – China imeishinda Ufaransa seti 3-0 na kunyakua taji lake la 11 mfululizo la mpira wa mezani duniani kwa timu za wanaume kwenye Fainali za Mashindano ya Mpira wa Mezani ya Timu ya Dunia ya Shirikisho la Mpira wa Mezani Duniani -- ITTF Busan 2024 siku ya Jumapili na kufikia rekodi ya mara 23 kwa China kubeba Kombe la Swaythling katika historia.

Wakikabiliana na Ufaransa, ambao walitinga fainali kwa mara ya kwanza tangu 1997, wachezaji watatu wa China, Fan Zhendong, Wang Chuqin na Ma Long waliisaidia China kunyoosha mwendelezo wake wa kutwaa taji katika michuano hiyo.

Wang akishindana katika ukumbi akiwa mchezaji wa kwanza, aliweka msingi wa ushindi mapema kwa kuonyesha uwezo wa kutawala katika mchezo wa kwanza kwa ushindi wa 11-4 dhidi ya mchezaji Felix Lebrun mwenye umri wa miaka 17.

Mchezaji huyo wa China ambaye ni wa pili kwa ubora duniani aliendeleza kucheza kwa kasi baada ya hapo, na kuibuka mshindi kwa 11-8, 11-3 katika michezo miwili iliyofuata na kumpita Lebrun ambaye ni sita kwa ubora duniani na kuiweka China kwenye ubao wa matokeo.

Fan na Alexis Lebrun, kaka mkubwa wa Felix, walikuwa wachezaji waliofuata kwenye meza. Fan alicheza kwa kasi na kuongoza kwa seti 8-4 katika mchezo wa kwanza, huku hatua yake ya kimchezo ikishuhudia kasi ikiongezeka kuelekea upande wa mpinzani wake.

Matumaini ya Ufaransa kubaki kwenye kuwania ubingwa yaliegemea kwenye mabega ya Simon Gauzy, lakini yalifutwa na mkongwe wa China, Ma Long, ambaye alikuwa ameshinda mechi zake zote nne dhidi ya Gauzy.

Ma baada ya kuanza kwa kususua alijipanga upya kutoka hapo na kumchukulia mpinzani wake kwa uthabiti kwenye mguu wa nyuma na kuvuta ushindi wa kuimarika tena wa seti 11-2, 11-4, 11-6.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha