

Lugha Nyingine
Mazungumzo ya raundi ya 12 ya China kuhusu makubaliano na WTO yafanyika UAE (2)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Februari 25, 2024 ikionyesha mazungumzo ya raundi ya 12 ya China kuhusu makubaliano na WTO uliofanyika Abu Dhabi, Falme za Kiarabu. (WTO/ Xinhua) |
DUBAI - Mazungumzo ya raundi ya 12 ya China kuhusu makubaliano na WTO umefanyika kuanzia Jumamosi hadi Jumapili huko Abu Dhabi ambapo ulilenga kujenga ufahamu wa jinsi biashara na ushiriki katika WTO unavyoweza kuhimiza maendeleo na unyumbufu wa uchumi, haswa kwa Nchi za Kiarabu.
China siku zote inaziunga mkono nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi za Kiarabu, kuunganishwa katika utaratibu wa biashara wa pande nyingi na kusisitiza kunufaisha dunia nzima kwa maendeleo yake yenyewe, amesema Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao alipohutubia hafla ya ufunguzi wa mazungumzo hayo.
China itaendelea kufanya ushirikiano wa Kusini na Kusini ndani ya mfumokazi wa utaratibu wa biashara wa pande nyingi, kuongeza uwazi, ujumuishaji, ushiriki wa wote na usawa wa utaratibu huo, kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia kwa hatua halisi, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya kimataifa yenye mustakabali wa pamoja wa maendeleo.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Morocco Ryad Mezzour amesema kuwa China ina umuhimu mkubwa katika utaratibu wa biashara wa pande nyingi na imetoa mchango chanya katika kudumisha utaratibu huo.
Kwenye hafla hiyo, Wang na Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala walitia saini Mkataba mpya wa Maelewano juu ya Mradi wa China.
Mradi huo uliozinduliwa Mwaka 2011, unalenga kuimarisha ushiriki wa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo katika WTO na kusaidia serikali zinazoidhinisha kujiunga na shirika hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma