

Lugha Nyingine
Wanaharakati wa dunia nzima watoa wito wa kuboresha usimamizi ili kukabiliana na changamoto za kiikolojia (3)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Februari 26, 2024 ikionyesha mandhari ya nje ya ukumbi wa Mkutano wa Sita wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA-6) mjini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu) |
NAIROBI – Kuifanyia mageuzi mikataba ya pande nyingi ya mazingira na kuhakikisha kwamba inaendana na azma ya kufikia mazingira ya kijani, yaliyo salama na jumuishi inapaswa kuwa kipaumbele kwa serikali na washirika wa sekta hiyo, wanaharakati wa mazingira wamesema siku ya Jumatatu wakati wakizungumza pembezoni mwa Mkutano wa Sita wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA-6) unaoendelea mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Wanaharakati hao wa mazingira ya kijani wamesisitiza kuwa utawala bora, uwajibikaji na ushiriki wa raia utaongeza hatua katika changamoto kuu za ikolojia.
Dalia Marquez Anez, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa United Youth in Action, taasisi ya ushawishi wa mazingira ya kimataifa, amesema kuwa mfumo thabiti na wenye ufanisi wa kimataifa ni muhimu katika kukabiliana na matishio makubwa kwa mazingira, ikiwa ni pamoja na taka za kemikali, upotevu wa bioanuai na majanga ya tabianchi.
"Tunaomba kuwepo kwa sheria jumuishi na zilizo wazi za kimataifa, ambazo utekelezaji wake utakuwa muhimu katika kutafuta suluhu ya uchafuzi wa mazingira unaodhuru mazingira na afya ya binadamu," Anez amesema.
Mashirika ya kiraia yanayowakilisha wanawake, vijana na jamii za wenyeji mwishoni mwa wiki yalifanya kongamano la mashauriano kujadili na kufikia makubaliano juu ya msimamo wa pamoja wa kuwasilisha kwa wajumbe wanaohudhuria UNEA-6.
Anez amesema kuwa wanaharakati wa mazingira wameunga mkono baadhi ya maazimio yanayotarajiwa katika UNEA-6, yanayogusa ubora wa hewa, kuharakishakuanzisha mkataba wa plastiki, na hatua zinazotia mkazo wenye nguvu katika misukosuko ya tabianchi na upotevu wa mazingira asilia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma