Maonyesho ya Meetings Africa 2024 yafunguliwa Johannesburg, Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2024
Maonyesho ya Meetings Africa 2024 yafunguliwa Johannesburg, Afrika Kusini
Watu wakishiriki kwenye maonyesho ya Meetings Africa 2024 mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Februari 27, 2024. (Picha na Shiraaz Mohamed/Xinhua)

JOHANNESBURG – Maonyesho ya Meetings Africa 2024, ambayo ni maonyesho ya biashara ya Afrika, yameanza Jumanne mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ambapo yamevutia kampuni 380 kutoka nchi 21 za Afrika kushiriki maonyesho hayo kuonyesha bidhaa na huduma zao.

"Katika miaka yake ya mwanzoni, kampuni nyingi zilizoshiriki zilikuwa za Afrika Kusini, huku kukiwa kampuni chache kutoka nchi nyingine za bara hilo. Katika miaka mingi iliyopita, tumefanikiwa kupanua maonyesho hayo, na leo, imekuwa ni maonyesho ya kweli ya Afrika," ameyasema Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini, Patricia de Lille kwenye hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo.

Maonyesho hayo ya kila mwaka yamekuwa jukwaa muhimu la kimkakati kwa mikutano na shughuli za biashara, na alama mahususi katika kuonyesha mafanikio ya sekta ya shughuli za biashara barani Afrika, De Lille amesema, huku akibainisha kuwa kampuni zipatazo 19 zinashiriki maonyesho hayo kwa mara kwanza mwaka huu.

Huku nchi 63 zikiwa wanunuzi, maonyesho ya Meetings Africa ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa shughuli kubwa ya kuungana mkono na kushirikiana ambao unaenea zaidi ya Bara la Afrika, kwa mujibu wa De Lille.

Maonyesho ya Meetings Africa yamekuwa yakifanyika kwa miaka 18 na mwaka huu ni wa 17 kufanyika kwake kwani yaliahirishwa Mwaka 2021 kutokana na janga la UVIKO-19. Maonyesho ya Meetings Africa 2024 yatakamilika leo Jumatano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha