

Lugha Nyingine
Misri yadondosha misaada ya kibinadamu kwa ndege za kijeshi mjini Gaza (4)
![]() |
Misaada ya kibinadamu iliyodondoshwa na ndege za kijeshi za Misri ikionekana juu ya Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 27, 2024. (Picha na Yasser Qudih/Xinhua) |
CAIRO – Ndege za Jeshi la Anga la Misri zimedondosha misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumanne, Televisheni ya Habari ya Al-Qahera ya Misri imeripoti ikinukuu chanzo cha ngazi ya juu cha usalama ambacho kimesema shughuli hiyo ya kudondosha misaada kutokea angani, ambao umefanywa kwa kushirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan, unahusisha vitu kama vile chakula na vifaa vya matibabu kwa ajili ya eneo hilo lililozuiliwa.
Waziri wa Mshikamano wa Kijamii wa Misri Nivine El-Kabbag alisema Februari 16 kwamba Misri ilituma karibu tani 200,000 za misaada ya kibinadamu huko Gaza, ambayo inachukua asilimia 60 ya misaada yote kutoka nchi zaidi ya 37.
Israel imekuwa ikilishambulia Kundi la Hamas huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023, baada ya kundi hilo kuvamia eneo la kusini mwa Israel na kuua watu takriban 1,400. Vizuizi vya Israel na mashambulizi ya anga yamesababisha vifo vya Wapalestina 29,878, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya inayosimamiwa na Kundi la Hamas iliyotolewa siku ya Jumanne.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma