Mahakama ya Juu ya Marekani yatoa hukumu kwamba Trump anaweza kushiriki kwenye uchaguzi wa awali wa Colorado (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2024
Mahakama ya Juu ya Marekani yatoa hukumu kwamba Trump anaweza kushiriki kwenye uchaguzi wa awali wa Colorado
Askari wakifanya doria nje ya Mahakama ya Juu ya Marekani mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 4, 2024. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Mahakama ya Juu ya Marekani Jumatatu imetoa uamuzi kwa kauli moja kwamba Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushiriki kwenye uchaguzi wa awali wa urais katika Jimbo la Colorado, ikikataa kuondolewa kwake kulikofanywa na jimbo hilo na kimsingi kuweka miongozo kwa majimbo ya nchi nzima ambapo majaji tisa, watatu wa mrengo wa kiliberali na sita wa mrengo wa kihafidhina, wote wamekubaliana na hukumu hiyo.

Uamuzi unasema kwamba majimbo hayana mamlaka ya kumwondoa Trump kwenye karatasi ya kura kutokana na kuhusika kwake katika matukio yaliyotangulia ghasia za kwenye Jengo la Bunge la Marekani, Capitol Januari 6, 2021, mahakama hiyo imetoa ushindi muhimu kwa rais huyo wa zamani, ambaye ndiye kinara katika mbio za kuteuliwa kugombea urais kupitia chama cha Republican.

Mahakama hiyo imetangaza kwamba Mahakama ya Juu ya Colorado ilikuwa na dhana isiyo sahihi kwamba majimbo yana mamlaka ya kuamua kama mgombea urais ataondolewa chini ya Kifungu cha 3 cha Marekebisho ya 14 ya Katiba, ambacho kinakataza watu ambao wamehusika katika uasi kushika madaraka ya umma.

"Kwa sababu Katiba inalifanya Bunge la Wawakilishi, badala ya majimbo, kuwajibika kutekeleza kifungu cha 3 dhidi ya wasimamizi na wagombea wote wa madaraka ya umma ya serikali kuu, tunatengua” hukumu hiyo inasomeka.

Uamuzi huo unaweka wazi kuwa ni Bunge la Wawakilishi, badala ya majimbo mahsusi, ndilo ambalo lina jukumu la kuweka kanuni kuhusu utekelezaji wa kifungu cha Marekebisho ya 14 ya Katiba.

Kwa hiyo, uamuzi huu unatumika kwa majimbo yote ya Marekani, si tu Colorado.

"USHINDI MKUBWA KWA MAREKANI!!!" Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii muda mfupi baada ya hukumu hiyo ya Mahakama ya Juu kutolewa.

Ofisa mkuu wa Jimbo la Colorado Jena Griswold ameeleza msikitiko wake juu ya hukumu hiyo. "Colorado inapaswa kuwa na uwezo wa kuzuia waasi wa kuvunja kiapo kutoka kwenye karatasi zetu za kura," ameandika kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kwa jina la Twitter.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha