Viongozi wa China na Afrika kukutana tena Beijing kujadili mipango ya maendeleo na ushirikiano wa siku zijazo

(CRI Online) Machi 07, 2024
Viongozi wa China na Afrika kukutana tena Beijing kujadili mipango ya maendeleo na ushirikiano wa siku zijazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akishiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu sera ya mambo ya nje na uhusiano wa nje wa China wakati mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China unapoendelea mjini Beijing, China, Machi 7, 2024. (Xinhua/Cai Yang)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema mkutano mwingine wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika nchini China mwaka huu, ambapo viongozi wa China na Afrika watakutana tena mjini Beijing baada ya miaka sita kujadili mipango ya ushirikiano wa maendeleo ya siku zijazo na kubadilishana kwa kina uzoefu katika utawala wa nchi.

Wang Yi amesema hivi sasa, “ulimwengu wa kusini” unaowakilishwa na China na Afrika unashamiri na una mchango mkubwa katika historia ya dunia na kwamba katika mchakato huu mpya wa kihistoria, China itaendelea kusimama kidete na ndugu wa Afrika, kuiunga mkono Afrika katika kujitegemea, , kuboresha uwezo wake wa kujiendeleza, na kuharakisha mchakato wake wa ujenzi wa mambo ya kisasa.

Amesema China daima imekuwa ikisisitiza kuwa Afrika haipaswi kutengwa.

Amesema baada ya ushirikiano kati ya China na Afrika kushamiri, nchi nyingine kubwa pia zimeelekeza tena nguvu zao kwa Afrika, na China inakaribisha hali hiyo.

Amesema China inatumai kuwa pande zote, kama ilivyo kwa China, zitaitilia maanani zaidi Afrika, kuongeza uwekezaji barani Afrika, na kuunga mkono maendeleo ya Afrika.

Amesema, China pia iko tayari kufanya ushirikiano zaidi wa pande tatu na wa pande nyingi kwa msingi wa kuheshimu matakwa ya Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha