Mradi mpya wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua unaoelea majini waonyesha ushirikiano kati ya China na Thailand katika nishati safi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2024
Mradi mpya wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua unaoelea majini waonyesha ushirikiano kati ya China na Thailand katika nishati safi
Picha iliyopigwa Machi 5, 2024 ikionyesha kituo cha kuzalisha umeme kwa mseto wa nishati ya jua na maji kinachoelea majini wa Bwawa la Ubolratana huko Khon Kaen, Thailand. (Xinhua/Lin Hao)

KHON KAEN, Thailand - Bwawa la Ubolratana ambalo ni kituo cha kuzalisha umeme kwa mseto wa nishati ya jua na maji kinachoelea majini kiliojengwa kwa pamoja na kampuni za China na Thailand kimeanza kufanya kazi ya kibiashara siku ya Jumanne ili kusaidia maendeleo ya Thailand ya nishati safi.

Bwawa hilo, lililoko katika Jimbo la Khon Kaen, Kaskazini Mashariki mwa Thailand, linajumuisha kwa pamoja paneli za kuzalisha umeme kwa jua zinazoelea, umeme safi unaozalishwa kwa maji, mifumo ya kuhifadhi nishati yenye ufanisi mkubwa, na mifumo ya teknolojia za kisasa za usimamizi wa nishati, kwa mujibu wa kanpuni ya Ushirikiano wa kimataifa wa Umeme ya Dongfang, ambayo ni moja ya watengenezaji wakubwa zaidi wa vifaa vya kuzalisha umeme duniani na limejenga mradi huo na mshirika wake wa Thailand.

Jiraporn Sirikum, naibu mkuu wa Mamlaka ya Kuzalisha Umeme ya Thailand (EGAT), amesema kujenga kituo cha mitambo inayoelea ya kuzalisha umeme kwa mseto wa nishati ya jua na maji ni hatua muhimu katika kuelekea uzalishaji wa nishati safi na utulivu wa nishati wa Thailand, na kupongeza kampuni za China na Thailand kwa uwezo wa kukamilisha mradi huo kabla ya muda uliopangwa.

"Hii inaonyesha dhamira ya kuhimiza nishati safi nchini Thailand. Tunatumai kwa dhati kuwa mitambo hiyo inayoelea ya kuzalisha umeme kwa nishati mseto ya jua na maji itasaidia kuongeza nishati safi kwa uchumi wajamii na jamii za wenyeji," Jiraporn amesema kwenye hafla ya uzinduzi wa kazi ya mradi huo.

Liu Hongmei, Konsuli Mkuu wa Ubalozi wa China huko Khon Kaen, amesema anaamini kwamba kuanza kufanya kazi ya kibiashara kwa mradi huo kutaleta ustawi zaidi kwa watu wa kaskazini-mashariki mwa Thailand na kuashiria hatua mpya ya uwekezaji wa kampuni za China katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha