Habari picha: Mwanamama Mwendeshaji wa kreni ya mnara kwenye eneo la ujenzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2024
Habari picha: Mwanamama Mwendeshaji wa kreni ya mnara kwenye eneo la ujenzi
Picha iliyopigwa Machi 6, 2024 ikimwonyesha Li Xinxiu akifanya kazi ndani ya chumba cha waendesha kreni kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa awamu ya pili (sehemu ya mashariki) wa Kituo cha Mambo ya Kifedha cha Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Li Xinxiu mwenye umri wa miaka 46, ni mwanamama mwendesha kreni za mnara anayefanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa awamu ya pili (sehemu ya mashariki) ya Kituo cha Mambo ya Kifedha cha Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Akiwa ameketi kwenye chumba cha waendesha kreni cha ukubwa wa mita za mraba mbili kwenye mwinuko wa mita 416.6 juu ya mnara kuu wa mradi huo, Li anaendesha mtambo wa kreni ili kuinua kishikizi, kuzungusha mkono, kuinua vifaa vya ujenzi na kuvipeleka hadi eneo lengwa kwa usahihi.

"Kwa waendeshaji wa kreni za mnara, usalama ndiyo msingi," anasema Li. "Ni muhimu kuweka umakini, uangalifu na subira."

Kuona majengo marefu yakiinuka kutoka ardhini, Li anahisi fahari kuwa anaweza kuwa sehemu yake. (Xinhua/Li Bo)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha