Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China lafanya kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wake mkuu wa mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2024
Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China lafanya kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wake mkuu wa mwaka
Kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 7, 2024. (Xinhua/Chen Yehua)

BEIJING - Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) Alhamisi lilifanya kikao chake cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wake mkuu wa mwaka, ambapo Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya baraza hilo alihudhuria kikao hicho.

Kwenye mkutano huo, wajumbe 14 wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC walitoa maoni yao.

Mjumbe Ning Jizhe alisema, ni lazima kutolewa kwa sera zaidi ili kudumisha ongezeko la uchumi kwa hatua madhubuti, na kufanya kila juhudi za kupanua mahitaji ya ndani.

Mjumbe Chen Qun amesema ni muhimu kutoa nafasi ya kutosha kwa utafutaji huria katika utafiti wa kimsingi, na kuwatia moyo watafiti kutafuta na kugundua masuala yenye thamani kuhusu sayansi na teknolojia.

Mjumbe Yi Gang ametoa wito wa kuhimiza kufunguliwa mlango kwenye kiwango cha juu katika sekta ya mambo ya fedha ili kulinda usalama wa mambo ya fedha na uchumi wa nchi.

Mjumbe Sima Hong amesema maendeleo yenye ubora wa hali ya juu yanahitaji kuungwa mkono na mfumo wa kisasa wa viwanda, akisisitiza haja ya kujenga mfumo wa viwanda wa kuongozwa na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na viwanda vya teknolojia ya hali ya juu vikiwa uti wa mgongo.

Mjumbe Che Jun akielezea maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Yangtze kama mamabo makubwa ya kufanywa, amesema jitihada zinapaswa kufanywa ili kuunganisha zaidi mikakati ya sehemu mbalimbali na kuhimiza ujenzi wa maeneo ya vielelezo.

Mjumbe Wang Lu amechangia maoni yake juu ya kuhimiza maendeleo ya viwanda vya nyenzo za aina mpya. Amesisitiza kuwa ni lazima kuharakisha kuunda muundo wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia unahusu kategoria kuu za nyenzo za aina mpya na makundi ya viwanda muhimu.

Washauri wengine wa kisiasa wamechangia maoni yao kuhusu ujenzi wa kilimo cha kisasa, aina mpya za matumizi katika manunuzi, uzalishaji wa nafaka, mfumo wa mambo ya fedha yanayohusiana na maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, pamoja na maoni kuhusu elimu, kampuni binafsi, huduma za utunzaji wa uzeeni, na huduma za uzazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha