Viwanda vya chai vyasaidia maendeleo ya jamii, kampuni huko Luzhou, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2024
Viwanda vya chai vyasaidia maendeleo ya jamii, kampuni huko Luzhou, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China
Watalii wakichuma majani ya chai kwenye bustani yenye mandhari ya chai katika Kijiji cha Meiling cha Wilaya ya Huguo ya Eneo la Naxi la Mji wa Luzhou katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China, Machi 10, 2024. (Xinhua/Jiang Hongjing)

LUZHOU - Katika miaka ya hivi karibuni, Eneo la Naxi la Mji wa Luzhou, katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China limefanya jihudi kubwa za kuendeleza upandaji wa chai katika majira ya mchipuko huku likiendeleza utalii wa chai.

Mashamba ya kupanda chai kwenye eneo hilo yamefikia ukubwa wa jumla wa hekta 21,000, Eneo la Naxi linaweza kuzalisha tani 23,000 za majani ya chai kila mwaka, na kuleta manufaa kwa familia zaidi ya 5,600, ambapo kampuni zaidi ya 100 za utengenezaji wa chai zimeanzishwa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha