Mandhari ya mashamba ya mimea ya rapa huko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2024
Mandhari ya mashamba ya mimea ya rapa huko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China
Picha iliyopigwa Machi 9, 2024 ikionyesha mandhari ya mashamba ya mimea ya rapa kwenye sehemu yenye mandhari nzuri ya Chongkan ya Eneo la Tongnan la Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China. (Xinhua/Wang Quanchao)

Eneo la Tongnan katika Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China linajivunia historia ndefu ya upandaji mimea ya rapa yenye kuzalisha mafuta ya kupika, na ilitambuliwa kuwa mji uanaoongoza utoaji wa mbegu za mimea ya rapa nchini humu Mwaka 2022. Serikali za mitaa za eneo hilo zimeanzisha shughuli za utalii na huduma husika ili kutumia ipasavyo thamani ya mashamba ya mimea ya rapa katika eneo hilo, hali ambayo imeongeza kipato cha wakulima na kuhimiza mchakato wa ustawishaji wa vijiji huko. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha