Teknolojia yawezesha watu wenye ulemavu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2024
Teknolojia yawezesha watu wenye ulemavu
Mbwa roboti ya kuongoza watu wenye ulemavu wa macho ikikutana na mbwa halisi wa kuongoza watu wenye ulemavu wa macho kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Huiai, tarehe 13, Machi.

Maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Huiai yaliyoandaliwa na Shirikisho la Watu wenye Ulemavu la Beijing yamefunguliwa tarehe 13, Machi kwenye Kituo cha Kielelezo cha Huduma za Watu wenye Ulemavu cha Beijing.

Aina zaidi ya 20 za bidhaa za teknolojia ya hali ya juu za usaidizi wa walemavu zilizozalishwa na kampuni za China, zikiwemo mbwa roboti ya kuongoza watu wenye ulemavu wa macho, mfumo wa kuelekeza njia ndani ya nyumba, mkalimani wa AI wa lugha za ishara za mikono, roboti ya mfumo wa mifupa ya nje, teknolojia ya mchangamano wa kompyuta na ubongo wa walemavu inayowawezesha kuishi maisha ya kawaida, mashine ya mikono inayotumia teknolojia ya akili na misheni nyingine kadha wa kadha zimeoneshwa kwenye maonesho hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha