Viwanda vya mashine za kilimo vyafanya kazi kikamilifu kukidhi mahitaji ya kilimo cha majira ya mchipuko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 15, 2024
Viwanda vya mashine za kilimo vyafanya kazi kikamilifu kukidhi mahitaji ya kilimo cha majira ya mchipuko
Mfanyakazi akifunga kifaa chenye mfumo wa urambazaji wa satelaiti wa Beidou kwenye karakana ya kampuni ya kutengeneza matrekta huko Jiamusi, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini mashariki mwa China, Machi 12, 2024. (Xinhua/Wang Jianwei)

Katika mkoa wa Heilongjiang ambao unaongoza kwa uzalishaji nafaka nchini China, unaojulikana kama "ghala la nafaka" la nchi hiyo, kampuni za kutengeneza mashine za kilimo zina pilika nyingi ili kukidhi mahitaji ya soko kwa ajili ya kilimo cha msimu wa mchipuko mwaka huu.

Katika Mji wa Jiamusi, huku kilimo cha kisayansi na matumizi ya mashine zenye teknolojia za kisasa za kilimo yamekuwa mtindo mpya mwaka huu, utengenezaji wa mashine za kilimo sasa umeongezwa na mambo ya teknolojia ya hali ya juu zaidi, kama vile mfumo wa urambazaji wa satelaiti wa Beidou. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha