Hafla ya kuutangaza Mto Liangma yafanyika Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2024
Hafla ya kuutangaza Mto Liangma yafanyika Beijing, China
Watalii wakipiga picha za taa ya jadi yenye umbo la samaki kwenye hafla kando ya Mto Liangma mjini Beijing, China, Machi 16, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

Hafla ya kuutangaza Mto Liangma imefanyika siku ya Jumamosi mjini Beijing. Mto Liangma unapitia maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na balozi za nchi za nje, hoteli za kimataifa, maduka makubwa, na mitaa ya kibiashara ya kisasa, ukiunganisha maeneo mbalimbali ya biashara za kimataifa mjini Beijing.

Mwaka 2019, eneo la Chaoyang la Beijing lilianza mradi wa maeneo kando ya Mto Liangma. Baada ya kuendelezwa na kuboreshwa mazingira kwa miaka miwili, Mto Liangma umebadilika kutoka njia ya maji hadi kuwa maeneo ya maji yenye mandhari ya kuvutia. Sasa imekuwa sehemu ya lazima ya kutembelewa na watalii mjini Beijing.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha