Sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko zafanyika Mkoa wa Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2024
Sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko zafanyika Mkoa wa Xizang, China
Wakulima wakishiriki katika sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko katika Mji mdogo wa Codoi katika Wilaya ya Lhunzhub ya Mji wa Lhasa, Mkoa wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China, Machi 16, 2024. (Xinhua/Zhang Rufeng)

Sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko zimefanyika katika Mkoa wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China siku ya Jumamosi ambapo wakulima wakiwa wameshikilia "chema" (sanduku la mbao lililojaa nafaka za rangi na unga wa shayiri, ikiashiria bahati nzuri na ustawi katika tamaduni za Watibet), waliimba nyimbo, na kugongeana bilauri za mvinyo ya shayiri. Sherehe hiyo ina umuhimu mkubwa kwani inaashiria mwanzo wa msimu wa kilimo cha mwaka mpya na hutumika kwa ajili ya kuombea hali ya hewa nzuri na mavuno mengi. Inachukuliwa kuwa ibada muhimu katika maeneo ya kilimo ya Xizang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha