Xi Jinping akagua Mji wa Changsha katika Mkoa wa Hunan katikati ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2024
Xi Jinping akagua Mji wa Changsha katika Mkoa wa Hunan katikati ya China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea kampasi ya Chuo Kikuu cha Kwanza cha Ualimu cha Hunan, na kufahamishwa kuhusu juhudi za chuo hicho katika kutumia rasilimali zinazohusiana na urithi wa Chama kwa matumizi makubwa na utiliaji maanani wake katika kuhimiza maadili mema kupitia elimu huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Machi 18, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

CHANGSHA - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya jumatatu amekagua Changsha, mji mkuu wa Mkoa wa Hunan katikati ya China, ambapo alitembelea kampasi ya Chuo Kikuu cha Kwanza cha Ualimu cha Hunan na kampuni ya vifaa vya betri.

Amefahamishwa kuhusu jitihada za chuo kikuu hicho katika kutumia rasilimali zinazohusiana na urithi wa Chama kwa matumizi makubwa, utiliaji maanani wake katika kuhimiza maadili mema kupitia elimu, na jitihada za serikali ya mtaa katika kuharakisha maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha