

Lugha Nyingine
Eneo la kielelezo la kaboni karibu sifuri katika Mkoa Hainan laonyesha mwenendo wa maendeleo ya kijani ya China (10)
![]() |
Picha iliyopigwa Machi 9, 2024 ikionyesha Kituo cha Vyombo vya Habari cha Baraza la Boao la Asia (BFA) baada ya kukarabatiwa na paneli za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika eneo la kielelezo la kaboni karibu sifuri la Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Pu Xiaoxu) |
BOAO, Hainan - Eneo la kielelezo la kaboni karibu sifuri limeanza kufanya kazi siku ya Jumatatu huko Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China ambapo hafla ya uzinduzi imefanyika katika Kisiwa cha Dongyu mjini Boao kwa ajili ya "Eneo la Kielelezo la kaboni karibu Sifuri” ambao ni mradi uliojengwa kwa pamoja na Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini na Vijijini ya China na serikali ya mkoa wa Hainan.
Kwa kujumuisha teknolojia za kupunguza utoaji hewa chafu na kuchukua mbinu na hatua mbalimbali za kibunifu, eneo hilo linaweza kufikia uwiano kati ya uzalishaji na matumizi ya nishati mpya.
Mradi huo unalenga kuonyesha dhana, teknolojia na utekelezaji wa China katika maendeleo ya kijani na utoaji kaboni chache kwa Dunia.
Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao (BFA) Mwaka 2024 utafanyika kuanzia Machi 26 hadi 29 huko Boao, ukijikita katika namna jumuiya ya kimataifa inaweza kufanya kazi pamoja ili kukabiliana na changamoto za pamoja na kubeba wajibu wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma