Kampuni ya China kujenga uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu kaskazini mwa Tanzania kwa ajili ya fainali za AFCON 2027

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2024
Kampuni ya China kujenga uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu kaskazini mwa Tanzania kwa ajili ya fainali za AFCON 2027
Wawakilishi wakihudhuria hafla ya kutia saini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu katika mji wa Arusha, jijini Dar es Salaam, Tanzania, Machi 19, 2024. (Xinhua)

ARUSHA, Tanzania - Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi wa Reli ya China (CRCEG) imetia saini makubaliano na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania siku Jumanne kujenga uwanja wa mpira wa miguu katika mji wa Arusha, Kaskazini mwa Tanzania kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

"Baada ya kukamilika kwake, uwanja huo hautatumika tu kwa michezo ya mpira wa miguu, lakini pia kwa shughuli za kibiashara na sherehe rasmi za serikali," Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Damas Ndumbaro amesema kwenye hafla hiyo ya utiaji saini.

Ndumbaro amesema uwanja huo utaendelea kuvutia watalii ili kukuza utalii wa Arusha, mji ambao pia unaojulikana kama mji mkuu wa safari, huku akiongeza kuwa utakuwa ni alama mpya kabisa.

Uwanja huo wenye uwezo wa kupokea watu 30,000, utakaojengwa kwenye ardhi yenye ukubwa wa hekta 14.57, utakidhi viwango vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), imesema taarifa ya wizara hiyo.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027, ambayo ni mashindano makubwa ya kimataifa ya soka kwa wanaume barani Afrika, pamoja na Kenya na Uganda.

Zhou Zejun, mhandisi mkuu wa CRCEG Afrika Mashariki, amesema hamasa ya usanifu wa uwanja huo inatokana na madini ya Tanzanite na Mlima Kilimanjaro, wakati rangi zake zinatokana na bendera ya Taifa ya Tanzania.

"Mtindo wa usanifu wa jumla ni mwepesi na rahisi, ukiunganisha kikamilifu mazingira na utamaduni wa wenyeji," Zhou amesema, huku akiongeza kuwa katika muundo huo, muundo mrefu wa chuma na boriti kubwa utatumika, ukifikia viti vyote na kuhakikisha mazingira mazuri ya kutazama kwa watazamaji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha