Maonyesho makubwa ya nishati ya jua barani Afrika yanaanza nchini Afrika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2024
Maonyesho makubwa ya nishati ya jua barani Afrika yanaanza nchini Afrika Kusini
Watu wakionekana kwenye banda la Kampuni ya BYD kwenye Maonyesho ya nishati ya jua na uhifadhi wa nishati ya Africa 2024 huko Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 18, 2024. (Xinhua/Zhang Yudong)

JOHANNESBURG - Maonyesho ya nishati ya jua na uhifadhi wa nishati ya Africa 2024, ambayo ni maonyesho makubwa ya nishati mbadala katika Bara la Afrika, yamefunguliwa siku ya Jumatatu huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Yakifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Gallagher, maonyesho hayo ya siku tatu yamevutia kampuni zaidi 350 za ndani na nje ya Afrika Kusini kuonyesha bidhaa zao, kwa mujibu wa Terrapinn, kampuni ya kuandaa matukio ya kimataifa.

"Tumefurahi sana kurejea mwaka huu, huku awamu hii yakiwa yamepangwa kuwa makubwa zaidi kuliko hapo awali. Katika nyakati hizi ngumu, ni muhimu kwa sekta ya nishati na nishati ya jua kuja pamoja na kuelekea mustakabali endelevu zaidi huku ikitafuta suluhu zenye uvumbuzi, " amesema Gina Bester, afisa wa Terrapinn.

Amesema kampuni kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini zinaonyesha bidhaa na suluhu mbalimbali za nishati, zikiwemo moduli na vijenzi vya vifaa vya nishati ya jua, uhifadhi wa nishati mbadala na vibadilishaji umeme, vifaa vya kuzalisha umeme, na teknolojia za kisasa katika sekta ya nishati ya jua.

Wakati wa maonyesho hayo, pia kutakuwa na majukwaa na makongamano huku kukiwa na washiriki kutoka serikalini na wahusika wakuu katika sekta ya nishati kutoka kote Afrika ili kujikita kwenye masuala muhimu zaidi katika sekta ya nishati barani Afrika, kwa mujibu wa Bester.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha