Jukwaa la Kimataifa kuhusu demokrasia lafanyika Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2024
Jukwaa la Kimataifa kuhusu demokrasia lafanyika Beijing, China
Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria kwenye mkutano wa tatu wa "Jukwaa la Demokrasia la Kimataifa: Mtazamo wa Maadili ya Pamoja ya Binadamu" na kutoa hotuba mjini Beijing, China, Machi 20, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING – Mkutano wa tatu wa Jukwaa la Demokrasia la Kimataifa: Mtazamo wa Maadili ya Pamoja ya Binadamu umefanyika Jumatano mjini Beijing ambapo Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba.

Wageni zaidi ya 200 kutoka nchi, maeneo na mashirika mbalimbali ya kimataifa walishiriki katika mijadala kuhusu mada mbalimbali zikiwemo za "Demokrasia na Usimamizi wa Zama za Sasa," "Demokrasia na Utawala wa Kisheria katika Zama za Kidijitali," "AI na Mustakabali wa Demokrasia" na "Demokrasia na Usimamizi wa Kimataifa katika Dunia yenye ncha nyingi."

Wamekubaliana kwamba demokrasia ni alama muhimu ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, ambayo ni utafutaji wa siku zote wa Chama cha CPC na watu wa China. Wageni hao wamesema, baada ya utafiti wa muda mrefu, China imeanzisha njia ya maendeleo ya demokrasia yenye umaalumu wa China, ambayo imelinda haki za kidemokrasia za watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China, na kutoa uungaji mkono mkubwa kwa ajili ya kuhimiza ustawishaji wa Taifa la China kwa pande zote kwa kupitia njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Huku wakisisitiza kwamba demokrasia ina thamani ya pamoja kwa binadamu wote, wageni hao wametoa wito wa kuheshimiwa kikamilifu kwa juhudi za nchi zinazoendelea za kutafuta, kuendeleza na kufikia demokrasia, kupinga vitendo vya kuzusha mafarakano, kueneza maoni ya upande mmoja tu, na kuharibu amani kwa jina la demokrasia.

Jukwaa hilo limeandaliwa na Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, na kushirikisha Taasisi Kuu ya Sayansi ya Jamii ya China, Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China na Kundi la Utangazaji wa Kimataifa la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha