Maofisa na wasomi wapongeza mchango wa BRI katika kukuza maendeleo nchini Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2024
Maofisa na wasomi wapongeza mchango wa BRI katika kukuza maendeleo nchini Ethiopia
Watu wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kongamano kuhusu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 20 Machi 2024. (Xinhua/Liu Fangqiang)

ADDIS ABABA - Viongozi na wasomi kutoka Ethiopia na China Jumatano kwenye kongamano moja kuhusu Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wamepongeza pendekezo hilo kwa mchango wake mkubwa katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Ethiopia na kwingineko.

Gebeyehu Ganga, mkurugenzi mkuu wa Masuala ya Mashariki ya Kati, Asia na Pasifiki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, alisisitiza kuwa pendekezo la BRI tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 limeendelezwa kuwa jukwaa la Dunia la ushirikiano wa kimataifa ulio wazi, jumuishi na kunufaishana.

"Tunapoingia katika muongo wake wa pili, BRI itaendelea kusukuma maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi zinazoshiriki, ikiwa ni pamoja na Ethiopia. Ethiopia ikiwa lango la Afrika, ni mtangulizi wa kupigiwa mfano wa ushirikiano kati ya China na Afrika, ikifanya kazi kama kitovu muhimu unganishi katika bara la Afrika na mwenzi thabiti wa China katika kuendeleza ushirikiano kupitia majukwaa ya pamoja," amesema kwenye kongamano hilo lililohudhuriwa na maofisa waandamizi wa Ethiopia na China, watu wa Ethiopia waliosoma China, pamoja na wasomi na wadau wengine kwa ujumla wapatao 50.

Ganga ameelezea manufaa halisi ya miradi ya miundombinu na njia za muunganisho nchini Ethiopia, hasa akitolea mfano njia ya reli ya SGR ya Ethiopia-Djibouti, ambayo imeboresha kwa kiasi kikubwa njia za kuagiza na kuuza nje za Ethiopia.

Amesema BRI ni muhimu katika kuchochea matarajio ya maendeleo ya Ethiopia kwa kusaidia kujenga maeneo ya viwanda na kuweka msingi wa ukuaji wa viwanda vya uzalishaji katika nchi hiyo.

Kongamano hilo lilitafakari mafanikio ya BRI katika mwongo mmoja uliopita na kujadili mikakati ya kuendeleza ajenda ya BRI yenye kiwango cha juu na uvumbuzi zaidi katika siku zijazo, ikilenga kuhimiza maendeleo yenye matokeo halisi na kunufaishana kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi hizo mbili.

Xu Jianping, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Ufunguaji mlango wa Kikanda katika Kamati ya Maendeleo ya Mageuzi ya Kina ya China, amesisitiza matokeo ya ushirikiano na China chini ya BRI nchini Ethiopia. Amesisitiza dhamira ya China ya kutekeleza ushirikiano wa kiwango cha juu wa BRI wakati ambapo pendekezo hilo linaingia muongo wake wa pili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha