Rais Xi Jinping atoa wito kwa Mkoa wa Hunan kuandika ukurasa wake mpya wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 22, 2024
Rais Xi Jinping atoa wito kwa Mkoa wa Hunan kuandika ukurasa wake mpya wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea kampasi ya Chuo Kikuu cha Kwanza cha Ualimu cha Hunan, na kufahamishwa kuhusu juhudi za chuo hicho katika kutumia rasilimali za urithi wa mali ya Chama kwa ajili ya kuhimiza maadili mema kupitia elimu huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Machi 18, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

CHANGSHA - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Hunan wa China kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi ametoa wito kwa mkoa huo kuendelea kujizatiti kwa mageuzi na uvumbuzi na kufuata hali halisi na kuchukua hatua zenye matokeo halisi ili kuandika ukurasa wake katika ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi ameutaka mkoa huo kujijenga kuwa kituo cha kitaifa cha viwanda muhimu na vya teknolojia ya hali ya juu na kituo cha sayansi na teknolojia na uvumbuzi chenye uwezo wa kimsingi wa ushindani, na kuendelea kuwa kichocheo cha mageuzi na ufunguaji mlango wa maeneo ya nchini China.

Katika ziara yake hiyo ya ukaguzi, Xi alikagua Chuo Kikuu cha Kwanza cha Ualimu cha Hunan katika Mji wa Changsha, kampuni ya vifaa vya betri iliyowekezwa kwa ubia na China na Ujerumani, alitembelea mtaa wa kitamaduni katika mji wa Changde, na kutembelea kijiji kimoja cha Changde.

Siku ya Alhamisi, baada ya kusikiliza ripoti ya maofisa viongozi wa Chama na serikali wa mkoa huo kuhusu kazi yao, Rais Xi ameongeza kazi ya Hunan.

Ametoa wito wa kuimarisha nafasi kuu ya kampuni katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na kuhimiza mafungamano ya pande zote ya minyororo ya uvumbuzi, viwanda, mtaji na rasilimali watu. Pia ametoa wito wa kuendeleza utafiti mkubwa wa teknolojia na vifaa na kuendeleza zaidi utengenezaji bidhaa unaotegemea teknolojia ya hali ya juu.

Kuhusu kuimarisha mageuzi, Rais Xi amesema mkazo unapaswa kuwekwa katika kutatua matatizo ambayo yanarudisha nyuma kustawisha mwelekeo mpya wa maendeleo na maendeleo yenye sifa nzuri. Amesema mageuzi lazima yatoe msukumo na uhai katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Rais Xi pia ameitaka Hunan kushiriki kwa pande zote katika ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuendeleza vyema eneo la majaribio ya biashara huria kwa vigezo vya juu, na kujitahidi kujenga eneo la majaribio la kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika uchumi na biashara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha