Maonyesho ya Picha yanayofanyika Nairobi yaonyesha ushirikiano kati ya China na Afrika chini ya BRI

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2024
Maonyesho ya Picha yanayofanyika Nairobi yaonyesha ushirikiano kati ya China na Afrika chini ya BRI
Watu wakitembelea Maonyesho ya Picha kuhusu Ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja mjini Nairobi, Kenya, tarehe 22 Machi 2024. (Xinhua/Han Xu)

Maonesho ya Picha yanayoonyesha mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) yameanzishwa Tarehe 22, Machi, huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Maonyesho hayo ya mwezi mmoja yamefanyika katika kituo cha Nairobi cha Reli ya Mombasa-Nairobi (SGR), yanaonyesha picha zaidi ya 30 kuhusu matokeo ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

Maonyesho hayo yenye mada ya “Hata milima na bahari haziwezi kuwatenganisha watu kwa matarajio ya pamoja, ” yanaonesha manufaa ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali.

Xu Jianping, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ufunguaji mlango ya Kikanda katika Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China, alipongeza ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika, hasa katika ujenzi wa miundombinu, kuandaa watu wenye ujuzi na sekta ya afya.

Philip Mainga, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli la Kenya, alisema maonyesho hayo ya picha yataonyesha mchango wa China katika maendeleo ya uchumi wa kisasa wa Kenya.

"Pendekezo la BRI limeleta mabadiliko katika nchi ya Kenya na bara la Afrika," Mainga alisema, akizungumzia miradi ya miundombinu iliyojengwa na China ambayo imeimarisha muunganisho na kuingiza uhai katika uchumi wa sehemu yetu ." Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja (BRI) limekuwa mradi wa mafanikio nchini Kenya. Tumeshuhudia miundombinu yetu kuboreshwa kwa kiasi kikubwa kupitia pendekezo hilo, kuongeza muunganisho kati ya miji na vijiji vyetu," alisema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha