Lugha Nyingine
Eneo Jipya la Xiong'an: Mji wa Siku za Baadaye wa China (9)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2024
Picha iliyopigwa Machi 29, 2024 ikionyesha Stesheni ya Reli ya Xiong'an katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Mu Yu) |
Mnamo Aprili 2017, China ilitangaza mpango wa kuanzisha Eneo Jipya la Xiong'an, ambalo linaunganisha wilaya tatu za Rongcheng, Anxin na Xiongxian, pamoja na baadhi ya maeneo yaliyo karibu nazo katika Mkoa wa Hebei Kaskazini mwa China.
Eneo hilo jipya linalenga kuondoa kazi zisizo za lazima za Mji wa Beijing kwa kulingana na hadhi yake ya kuwa mji mkuu wa China, wakati huohuo kuendeleza maendeleo yanayoratibiwa ya eneo la Beijing-Tianjin-Hebei.
Nchi ya China pia imejipanga kuijenga Xiong'an, iliyopewa jina la "mji wa siku za baadaye," kuwa mji wa uvumbuzi , wa kijani, wenye teknolojia za kisasa na wa hadhi ya kimataifa ukiwa na anga la buluu, hewa safi na maji safi, ili kuendana na njia ya maendeleo yenye ubora wa juu ya China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma