Lugha Nyingine
Jukwaa la Boao la Asia lafanya mkutano na waandishi wa habari wa kufunga mkutano wake wa mwaka 2024 (2)
Picha iliyopigwa tarehe 29, Machi ikionesha mkutano na waandishi wa habari wa kufunga Baraza la Boao la Asia. (Picha na Guo Cheng/Xinhua) |
Baraza la Boao la Asia lilifanya mkutano na waandishi wa habari wa kufunga mkutano wake wa mwaka wa 2024 Ijumaa Machi 29 kwenye Kituo cha Vyombo vya Habari cha Baraza la Boao ambapo Katibu Mkuu wake Li Baodong ametoa shukrani zake za dhati kwa wawakilishi kutoka kote duniani waliofika Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China kuhudhuria mkutano huo wa mwaka huu.
Li amesema kuwa, mkutano wa mwaka huu ni mkutano wa kwanza wa mwaka baada ya kuzinduliwa kwa Eneo la Kielelezo la Kaboni-Sifuri la Jukwaa la Boao la Asia. Mkutano huo umehimiza sana ushirikiano wa kijani, na kuhimiza uhifadhi wa nishati na upunguzaji wa hewa chafu kupitia ujenzi wa kijani, ugavi wa kijani, usafiri wa kijani, mawasiliano ya kijani, kukabiliana na kaboni ya bluu na njia nyingine.
Amesema, washiriki wote wanaamini kuwa mada ya mkutano wa mwaka huu ya "Asia na Dunia: Changamoto za Pamoja, Kuchangia Wajibu" inaakisi matatizo muhimu zaidi duniani, na pia inaakisi juhudi zinazofanywa na Baraza hilo katika kuhimiza ushirikiano wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma