Ban Ki-moon: Tunakabiliwa na changamoto za pamoja, tunapaswa kuchangia wajibu

By Aris (Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2024
Ban Ki-moon: Tunakabiliwa na changamoto za pamoja, tunapaswa kuchangia wajibu
Ban Ki-moon, mwenyekiti wa Baraza la Boao la Asia (BFA) na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, akihutubia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 mjini Boao, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Machi 28, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)

Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa nane wa Umoja wa Mataifa wakati akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2024 asubuhi ya Machi 28 mjini Boao, China, amerejelea changamoto zinazoikabili Dunia ya leo na kuhimiza wageni wanaohudhuria mkutano huo kufikiria kwa namna mbalimbali juu ya uhalisia wa hali na kuunda mustakabali wa siku za baadaye kwa vitendo vyenye kuwajibika.

Ban Ki-moon ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Boao la Asia amekumbusha kuwa kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi kumemwezesha kushuhudia nyakati nzuri na nyakati ngumu. Amesema wakati "nyakati nzuri" zinapokuja, dunia inafurahia faida za gawio la amani duniani na utandawazi wa haraka; wakati "nyakati mbaya" zinapokuja, Dunia hugawanyika katika kambi na makundi yanayopingana.

"Hatupaswi kurudi kwenye 'siku mbaya' kwa namna yoyote, na njia pekee ya kusonga mbele ni mshikamano, ushirikiano, uhusiano wa pande nyingi, utandawazi, na uchumi wa dunia ulio wazi" amesisitiza.

Ban Ki-moon amesema kuwa msukosuko wa dunia unailazimisha dunia kufanya kazi pamoja huku akisisitiza kuwa wakati wa kukabiliana na changamoto za pamoja dunia inapaswa pia kuchangia wajibu.

Ametoa wito kwa viongozi wa Asia na Dunia waliopo kwenye Baraza la Boao kusimama, kusema kile kinachopaswa kusemwa, na kutenda kwa uamuzi, ili kujenga mustakabali wa siku za baadaye kwa maneno na vitendo na kuishi kulingana na matarajio ya watu.

Akihitimisha hotuba yake amesema kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi lilizifanya nchi kuweza kufikia makubaliano ya kihistoria katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, lakini hali halisi inahitaji Dunia kuchukua hatua madhubuti zaidi ili kupiga hatua zaidi.

Amesema, mwenendo wa hali isiyo na uhakika katika siasa za kijiografia na uchumi wa kijiografia vinaleta wasiwasi; minyororo ya ugavi, biashara na mtiririko wa uwekezaji wa kimataifa unapangwa upya, na utandawazi jumuishi unatolewa kafara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha