Mji wa Shenzhen wafanya juhudi kusaidia vijana wenye tatizo la usonji kujiunga na jamii na kufuata matumaini (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 02, 2024
Mji wa Shenzhen wafanya juhudi kusaidia vijana wenye tatizo la usonji kujiunga na jamii na kufuata matumaini
Dai Jinyu, kijana mwenye umri wa miaka 29 mwenye tatizo la usonji akifanya kazi katika Jumuiya ya Watu wenye Tatizo la Usonji ya Shenzhen huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Machi 27, 2024. (Xinhua/Mao Siqian)

Wu Huajian mwenye umri wa miaka 19, na Xu Jilun mwenye umri wa miaka 30, wamekuwa wakifanya kazi katika kituo cha kuosha magari huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China tangu Julai 2023. Wafanyakazi jumla ya 15 wenye ulemavu wa akili kwa sasa wanafanya kazi hapa. Leo Jumanne ni siku ya maadhimisho ya 17 ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Usonji. Katika Mji wa Shenzhen, Kusini mwa China, baadhi ya vijana wenye usonji, ambao wanaitwa "watoto wa nyota," wamejiunga na jamii na kufuata matumaini yao.

Katika miaka ya hivi karibuni, watoto wenye usonji nchini China wamepata uangalizi na matunzo yanayoongezeka. Mwaka 2022, Kamati ya Kitaifa ya Matibabu na Afya ya China ilitoa itifaki ya majaribio ya uchunguzi wa usonji na huduma za kuingilia kati kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka sita ili kuboresha huduma zinazohusika. Na serikali ya China pia imetoa mpango kazi wa kuboresha elimu maalum katika kipindi cha Mpango wa 14 wa maendeleo ya uchumi na jamii ya miaka mitano (2021-2025). (Xinhua/Mao Siqian)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha