

Lugha Nyingine
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Ufaransa wafanya mazungumzo (2)
![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Stephane Sejourne, Waziri wa Mambo ya Ulaya na ya Nje wa Ufaransa, mjini Beijing, China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan) |
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Stephane Sejourne, Waziri wa Mambo ya Ulaya na ya Nje wa Ufaransa, mjini Beijing siku ya Jumatatu na kujadili uhusiano wa karibu kati ya pande mbili ambapo amesema kuwa China na Ufaransa zote ni wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa zinazojitegemea, na kwamba zinachangia historia maalum ya mawasiliano na kubeba wajibu muhimu wa zama hizo.
Huku akibainisha kuwa mwaka huu ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya China na Ufaransa, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema China ingependa kushirikiana na Ufaransa ili kuimarisha na kuongeza nguvu kwenye ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ufaransa, ukielekezwa na makubaliano ya kimkakati yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.
Amesema China inapenda kuelekeza maendeleo mazuri na thabiti ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya na kuingiza utulivu zaidi katika Dunia inayokumbwa na misukosuko ya mara kwa mara.
Amesema China inaendeleza kikamilifu nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu. Amesema, hatua hizi zitaleta fursa zaidi kwa Ufaransa na Dunia nzima, na kuingiza uhai mpya katika uhusiano kati ya China na Ufaransa.
"Mawasiliano ya kimkakati na uratibu wa pande nyingi ni mambo muhimu ya ushirikiano kati ya China na Ufaransa," Wang amesema, huku akiongeza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kushirikiana ili kuzungumza juu ya masuala ya amani na utulivu wa Dunia, na masuala yanayohusiana na mustakabali wa binadamu. Amesema, pande hizo mbili zinapaswa pia kuungana mkono katika mipango ya pande nyingi yaliyotolewa na kila upande.
Sejourne amesema kuwa Ufaransa inatilia maanani sana uhusiano kati yake na China na inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Amesema, Ufaransa inatarajia kushirikiana na China kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, kuimarisha mawasiliano kati ya watu na watu, kusukuma mbele maendeleo zaidi ya uhusiano wa pande mbili, na kuimarisha ushirikiano katika nyanja kama vile uchumi, biashara, kilimo, maendeleo ya kijani na teknolojia za akili bandia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma