Siku ya Kimataifa ya Uelewa wa Usonji yaadhimishwa katika shule ya chekechea ya Beijing, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2024
Siku ya Kimataifa ya Uelewa wa Usonji yaadhimishwa katika shule ya chekechea ya Beijing, China
Walimu wakicheza michezo na watoto katika Shule ya Chekechea ya Kituo cha Sayansi ya Afya cha Chuo Kikuu cha Beijing cha China Machi 27, 2024. (Xinhua/Ren Chao)

BEIJING – Tukio lenye mada maalum limefanyika katika Shule ya Chekechea ya Kituo cha Sayansi ya Afya cha Chuo Kikuu cha Beijing cha China siku ya Jumanne, ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa wa Usonji mwaka huu, ili kuwasilisha nia njema na matunzo kwa watoto wenye usonji na familia zao kupitia shughuli mbalimbali kama vile ufundi wa kazi za mikono, uchezaji ngoma, maonyesho ya picha za watoto, na shughuli nyinginezo.

Shule ya Chekechea ya Kituo cha Sayansi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Beijing cha China imekuwa ikitekeleza elimu jumuishi tangu Mwaka 2007. Katika madarasa mengi ya shule hii maalum ya chekechea, watoto wenye usonji wanafurahia masomo na michezo pamoja na watoto wa kawaida.

Kwa sasa, shule hiyo ya chekechea imeanzisha mfumo maalum wa usaidizi kwa elimu ya awali ya watoto wenye usonji katika mambo ya utamaduni wa shule, wafanyakazi wa kufundisha, maeneo na vifaa vya watoto.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha