Kutana na Polisi Mbwa Corgi wa kwanza nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 09, 2024
Kutana na Polisi Mbwa Corgi wa kwanza nchini China
Fu Zai, mbwa corgi wa miezi sita akishiriki kwenye kipindi cha mafunzo huko Weifang, Mkoa wa Shandong wa China, Aprili 7, 2024. (Picha na Sun Shubao/Xinhua)

Akivunja dhana ya kawaida waliyonayo watu kuhusu mbwa mdogo, Fu Zai yuko tayari kunusa hatari akiwa ni mbwa wa polisi wa kwanza wa aina yake nchini China.

Mbwa huyo jamii ya Corgi anayependeza, hivi karibuni baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza katika shughuli ya wazi kwa umma iliyofanyika katika kambi ya polisi mjini Weifang, Mkoa wa Shandong wa China alivutia ufuatiliaji mkubwa mtandaoni kwa sababu ya uso wake wa tabasamu, "miguu mifupi" mizuri na stadi bora katika kutafuta mabomu.

Fu Zai alionyesha uwezo wake wa kipekee na kufanya kazi vizuri kama "mwanafunzi mwenye alama A" wakati wote katika siku zake za mwanzo za mafunzo.

Ingawa ameorodheshwa kama mbwa polisi wa akiba, Fu Zai bado anabeba majukumu makubwa ya kazi, akishiriki kwenye vipindi vya mafunzo vinavyohusisha mazoezi ya utii, utafutaji wa mabomu na ufuataji wa harufu, ambavyo vimepangwa kuwa vikifanyika kila asubuhi na alasiri.

Baada ya miezi minne ya mafunzo, hivi sasa Fu Zai anaweza kutambaa chini ya magari kwa ajili ya uchunguzi, au kuingia kwa urahisi kwenye nafasi nyembamba kwa kutumia miguu yake mifupi na umbo lake dogo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha