Kituo cha kuhifadhi nishati kwa hewa iliyogandamizwa chenye uwezo MW 300 chaanza kufanya kazi mkoani Hubei, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2024
Kituo cha kuhifadhi nishati kwa hewa iliyogandamizwa chenye uwezo MW 300 chaanza kufanya kazi mkoani Hubei, China
Picha iliyopigwa tarehe 9, Aprili 2024 ikionyesha mandhari ya kituo cha kuhifadhi nishati kwa hewa iliyogandamizwa chenye uwezo wa MW 300 huko Yingcheng, Mkoa wa Hubei, Katikati mwa China. (Xinhua/Cheng Min)

Kituo cha kuhifadhi nishati kwa hewa iliyogandamziwa chenye uwezo wa MW 300 katika Mji wa Yingcheng, Mkoa wa Hubei, Katikati mwa China kimeanza kufanya kazi rasmi siku ya Jumanne.

Huku kikiwa na teknolojia inayojulikana kwa jina la "kuhifadhi nishati kwa hewa iliyogandamizwa''. Katika wakati mahitaji ya umeme yakiwa ni madogo, hewa zitasukumwa kwa pampu na kuingia kwenye pango la chini ya ardhi, na wakati mahitaji ya umeme yakiongezeka hewa zitatolewa ili kuzalisha umeme.

Kikiwa kimepewa jina la "benki kubwa ya nishati", kituo hicho kinatarajiwa kuzalisha umeme wa kWh milioni 500 kwa mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha